Matukio Katika Picha: Uzinduzi wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini - Viwanja vya Ngongo
05 Aug 2026
Lindi Mwambao Cooperative Union (LMCU) imeshiriki kikamilifu katika Uzinduzi wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini, yaliyofanyika katika Viwanja vya Ngongo. Uzinduzi huu umeambatana na ushiriki wa viongozi wa serikali, wadau wa sekta ya kilimo, na wanachama wa vyama vya ushirika kutoka mikoa ya Kanda ya Kusini.
LMCU inaendelea kushiriki matukio ya kitaifa yanayolenga kuinua sekta ya kilimo na ushirika nchini, ikiwemo kuonesha mchango wa zao la korosho katika uchumi wa wanachama na taifa kwa ujumla.








